Zab 27 - Swahili Union Version Bible

Wimbo wa Ushindi katika Bwana wa DaudiYa Daudi.

1BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,

Nimwogope nani?

BWANA ni ngome ya uzima wangu,

Nimhofu nani?

2Watenda mabaya waliponikaribia,

Wanile nyama yangu,

Watesi wangu na adui zangu,

Walijikwaa wakaanguka.

3Jeshi lijapojipanga kupigana nami,

Moyo wangu hautaogopa.

Vita vijaponitokea,

Hata hapo nitatumaini.

4Neno Moja nimelitaka kwa BWANA,

Nalo ndilo nitakalolitafuta,

Nikae nyumbani mwa BWANA

Siku zote za maisha yangu,

Niutazame uzuri wa BWANA,

Na kutafakari hekaluni mwake.

5 Mit 18:10; Isa 4:6; Kol 3:3 Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,

Atanisitiri katika sitara ya hema yake,

Na kuniinua juu ya mwamba.

6Na sasa kichwa changu kitainuka

Juu ya adui zangu wanaonizunguka.

Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;

Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.

7Ee BWANA, usikie, kwa sauti yangu ninalia,

Unifadhili, unijibu.

8Uliposema, Nitafuteni uso wangu,

Moyo wangu umekuambia,

BWANA, uso wako nitautafuta.

9Usinifiche uso wako,

Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.

Umekuwa msaada wangu, usinitupe,

Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu.

10 Isa 49:15; Yn 16:32; 2 Tim 4:16-18 Baba yangu na mama yangu wameniacha,

Bali BWANA atanikaribisha kwake.

11Ee BWANA, unifundishe njia yako,

Na kuniongoza katika njia iliyonyoka;

Kwa sababu yao wanaoniotea;

12 1 Sam 22:9; Mt 26:59,60 Usinitie katika nia ya watesi wangu;

Maana mashahidi wa uongo wameniondokea,

Nao watoao jeuri kama pumzi.

13 Zab 112:7,8 Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA

Katika nchi ya walio hai.

14 Zab 62:1,5; Isa 25:9; Hab 2:3 Umngoje BWANA, uwe hodari,

Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help