Zab 83 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Hukumu dhidi ya adui wa IsraeliWimbo. Zaburi ya Asafu.

1Ee Mungu, usistarehe,

Ee Mungu, usinyamae, wala usitulie.

2 Zab 2:1 Maana adui zako wanafanya ghasia,

Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao.

3 Zab 27:5; Kol 3:3 Juu ya watu wako wanafanya hila,

Na kushauriana juu yao uliowaficha.

4 2 Sam 10:6; 2 Nya 20:1 Wamesema, Njoni, tuwakatilie mbali wasiwe taifa,

Na jina la Israeli halitakumbukwa tena.

5Maana wanashauriana kwa moyo mmoja,

Juu yako wanafanyana agano.

6Hema za Edomu, na Waishmaeli,

Na Moabu, na Wahagari,

7Gebali, na Amoni, na Amaleki,

Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,

8Ashuri naye amepatana nao,

Wamewasaidia wana wa Lutu.

9 Hes 31:7,8; Isa 9:4; Amu 4:6-22; 7:1-23 Uwatende kama Midiani, kama Sisera,

Kama Yabini, penye kijito Kishoni.

10Ambao waliangamizwa Endori;

Wakawa samadi juu ya nchi.

11 Amu 7:25; 8:12 Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,

Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna.

12Ambao Walisema,

Na tutamalaki makao ya Mungu.

13Ee Mungu, uwafanye kama mavumbi ya kisulisuli,

Mithili ya makapi mbele ya upepo,

14Kama moto uteketezao msitu,

Kama miali ya moto iiwashayo milima,

15Ndivyo utakavyowafuatia kwa tufani yako,

Na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

16Uwajaze nyuso zao fedheha;

Wakalitafute jina lako, BWANA.

17Waaibike, wafadhaike milele,

Naam, watahayarike na kupotea.

18Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA,

Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help