1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4 Isa 8:7; Ufu 22:1; 2 Nya 6:6; Zab 48:1; Isa 60:14; Ebr 12:22 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.
5 Kum 23:14; Isa 12:6; Eze 43:7 Mungu yu katikati yake hautatetemeshwa;
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki;
Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.
7BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8Njoni myatazame matendo ya BWANA,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;
Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,
Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
11BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.