1 Zab 2:5 BWANA, ni nani atakayekaa
Katika hema yako?
Ni nani atakayefanya maskani yake
Katika kilima chako kitakatifu?
2 Zab 84:11; Isa 33:15,16 Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,
Na kutenda haki.
Asemaye kweli kwa moyo wake,
3Asiyesingizia kwa ulimi wake.
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
4 Yos 9:18-20 Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,
Bali huwaheshimu wamchao BWANA
Ingawa ameapa kwa hasara yake,
Hayabadili maneno yake.
5 Eze 18:8,9 Hakutoa fedha yake apate kula riba,
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.