Mt 4 - Swahili Union Version Bible

Majaribu ya Yesu

1 Mk 1:12,13; Lk 4:1-13 Ebr 2:18; 4:15 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.

2Kut 34:28; 1 Fal 19:8Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

3Mwa 3:1-7Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

4Kum 8:3Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

5Mt 27:53Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,

6Zab 91:11-12akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,

Atakuagizia malaika zake;

Na mikononi mwao watakuchukua;

Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.

7 Kum 6:16 Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,

9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.

10Kum 6:13Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

11Yn 1:51; Ebr 1:6,14Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Yesu Aanza Huduma yake katika Galilaya

12 Mk 1:14,15; Lk 4:14,15 Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;

13Yn 2:12akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;

14Isa 8:13; 9:1ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,

15 Isa 8:22—9:1 Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,

Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani,

Galilaya ya mataifa,

16Watu wale waliokaa katika giza

Wameona mwanga mkuu,

Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti

Mwanga umewazukia.

17 Mt 3:2 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Yesu Awaita Wanafunzi wa Kwanza

18 Mk 1:16-20; Lk 5:1-11 Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Yn 1:40

19Mt 13:47; Eze 47:10Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.

20Mt 19:27Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.

21Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.

22Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.

Yesu Awahudumia Makundi ya Watu

23 Mt 9:35; Mk 1:39; Lk 4:15,44; Mdo 10:38 Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.

24Mk 6:55Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.

25Mk 3:7,8; Lk 6:17-19Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help