Zab 23 - Swahili Union Version Bible

Mchungaji MwemaZaburi ya Daudi.

1 Yn 10:11; 1 Pet 2:25 BWANA ndiye mchungaji wangu,

Sitapungukiwa na kitu.

2 Ufu 7:17; Eze 34:14 Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,

Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

3Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza

Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

4 Zab 46:11; Isa 8:10; Zek 8:23; Mt 1:23; Mdo 18:9,10 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,

Sitaogopa mabaya;

Kwa maana Wewe upo pamoja nami,

Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangu,

Machoni pa watesi wangu.

Umenipaka mafuta kichwani pangu,

Na kikombe changu kinafurika.

6 2 Kor 5:1 Hakika wema na fadhili zitanifuata

Siku zote za maisha yangu;

Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help