Isa 27 - Swahili Union Version Bible

Ukombozi wa Israeli

1 Eze 29:3; Ayu 41:1; Zab 74:14; 104:26 Katika siku hiyo BWANA, kwa upanga wake ulio mkali, ulio mkubwa, ulio na nguvu, atamwadhibu lewiathani, nyoka yule mwepesi, na lewiathani, nyoka yule mwenye kuzonga-zonga; naye atamwua yule joka aliye baharini.

2Katika siku hiyo; Shamba la mizabibu la mvinyo, liimbieni.

3Mimi, BWANA, nalilinda,

Nitalitia maji kila dakika,

Asije mtu akaliharibu;

Usiku na mchana nitalilinda.

4 2 Sam 23:6 Hasira sinayo ndani yangu;

Kama mibigili na miiba ingekuwa mbele zangu,

Ningepanga vita juu yake,

Ningeiteketeza yote pamoja.

5 Ayu 22:21; Isa 53:4,5; Efe 2:12-14 Au azishike nguvu zangu,

Afanye amani nami;

Naam, afanye amani nami.

6 Isa 37:31; Hos 14:5,6 Siku zijazo Yakobo atatia mizizi;

Israeli atatoa maua na kuchipuka;

Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.

7Je! Amempiga kama hilo pigo la hao waliompiga, au ameuawa kama walivyouawa wao waliouawa na yeye?

8Ayu 23:6; Zab 6:1; Yer 10:24; 1 Kor 10:13Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.

9Basi, uovu wa Yakobo utatakaswa hivyo, na hayo ndiyo matunda yote ya kumwondolea dhambi yake; afanyapo mawe yote ya madhabahu kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa, hata maashera na sanamu za jua havitasimama tena.

10Isa 17:2Kwa maana mji ulio na boma umekuwa peke yake, makao yaliyoachwa na ukiwa kama jangwa; huko ndiko atakakolisha ndama, na huko ndiko atakakolala, na kuyala matawi yake.

11Kum 32:18,28; Zab 28:5; Isa 1:3; 44:2,21,24; Yer 4:22; 2 The 1:8Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.

12Tena itakuwa katika siku hiyo, BWANA atayapiga-piga matunda yake toka gharika ya Mto hata kijito cha Misri, nanyi mtakusanywa mmoja mmoja, enyi wana wa Israeli.

13 Isa 2:11; Hes 10:2; Zab 81:3; Hos 8:1; Mt 24:31; Ufu 11:15 Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu na kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help