Zab 125 - Swahili Union Version Bible

Usalama wa Watu wa MunguWimbo wa kupanda mlima.

1Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,

Ambao hautatikisika, wakaa milele.

2Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,

Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,

Tangu sasa na hata milele.

3Kwa maana fimbo ya udhalimu

Haitakaa juu ya fungu la wenye haki;

Wenye haki wasije wakainyosha

Mikono yao kwenye upotovu.

4Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,

Nao walio wanyofu wa moyo.

5 Mit 2:15; Isa 59:8; Flp 2:15; Gal 6:16 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,

BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.

Amani ikae na Israeli.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help