Hos 12 - Swahili Union Version Bible

1 2 Fal 17:4; Isa 30:6 Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.

Uasi wa Muda Mrefu

2BWANA naye ana mateto na Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.

3 Mwa 25:26 Mwa 32:24-26 Tumboni alimshika ndugu yake kisigino;

Na alipokuwa mtu mzima alikuwa na uwezo kwa Mungu;

4 Mwa 28:10-22 Naam, alikuwa na uwezo juu ya malaika

Akashinda; alilia, na kumsihi;

Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;

5Naam, BWANA, Mungu wa majeshi;

BWANA ndilo kumbukumbu lake.

6Basi, mrudie Mungu wako; shika fadhili na hukumu; ukamngojee Mungu wako daima.

7Ni mchuuzi, mizani ya udanganyifu i mkononi mwake; anapenda kudhulumu.

8Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wo wote uliokuwa dhambi.

9Law 23:42-43Lakini mimi ni BWANA, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za karamu ya idi.

10Tena nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano.

11Amo 4:4Je! Gileadi ni uovu? Wamekuwa ubatili tu; huko Gilgali hutoa dhabihu za ng’ombe; naam, madhabahu zao zimekuwa kama chungu katika matuta ya mashamba.

12 Mwa 29:1-20 Na Yakobo alikimbia mpaka Padan-Aramu,

Na Israeli alitumika apate mke;

Ili apate mke alichunga kondoo.

13 Kut 12:50-51 Na kwa nabii BWANA alimtoa Israeli katika Misri,

Na kwa mkono wa nabii alihifadhiwa.

14 Kum 28:37; Dan 11:18 Efraimu amenitia hasira kali sana; kwa sababu hiyo damu yake itaachwa juu yake, na Bwana wake atamrudishia lawama yake.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help