Yn 12 - Swahili Union Version Bible

Mariamu Ampaka Yesu Mafuta

1 Mt 26:6-13; Mk 14:3-9 Yn 11:1,43 Basi, siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alifika Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye Yesu alimfufua katika wafu.

2Lk 10:40Basi wakamwandalia karamu huko; naye Martha akatumikia; na Lazaro alikuwa mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja naye.

3Lk 7:38Basi Mariamu akatwaa ratli ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.

4Basi Yuda Iskariote, mmojawapo wa wanafunzi wake, ambaye ndiye atakaye kumsaliti, akasema,

5Mbona marhamu hii haikuuzwa kwa dinari mia tatu, wakapewa maskini?

6Lk 8:3Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini; bali kwa kuwa ni mwivi, naye ndiye aliyeshika mfuko, akavichukua vilivyotiwa humo.

7Basi Yesu alisema, Mwache aiweke kwa siku ya maziko yangu.

8Kum 15:11Kwa maana maskini mnao sikuzote pamoja nanyi; bali mimi hamnami sikuzote.

Njama za Kumwua Lazaro

9Basi watu wengi katika Wayahudi walipata kujua ya kuwa yeye yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili yake Yesu tu, ila wamwone na Lazaro, ambaye Yesu alimfufua katika wafu.

10Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri la kumwua Lazaro naye;

11maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walijitenga, wakamwamini Yesu.

Yesu Aingia Yerusalemu kwa Ushindi

12 Mt 21:1-11; Mk 11:1-10; Lk 19:29-40 Nayo siku ya pili yake watu wengi walioijia sikukuu walisikia ya kwamba Yesu anakuja Yerusalemu;

13Zab 118:25,26wakatwaa matawi ya mitende, wakatoka nje kwenda kumlaki, wakapiga makelele, Hosana! Ndiye mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli!

14Zek 9:9Naye Yesu alikuwa amepata mwana-punda, akampanda, kama vile iliyoandikwa,

15Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.

16Yn 7:39Mambo hayo wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kwamba ameandikiwa hayo, na ya kwamba walimtendea hayo.

17Basi wakamshuhudia wale mkutano waliokuwapo pamoja naye alipomwita Lazaro kutoka kaburini, akamfufua.

18Na kwa sababu hiyo mkutano walikwenda kumlaki, kwa kuwa wamesikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.

19Yn 11:48Basi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno lo lote; tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.

Baadhi ya Wagiriki Wataka Kumwona Yesu

20 Yn 7:35; 11:55 Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwea kwenda kuabudu kwenye sikukuu.

21Yn 1:44; Lk 19:3; 23:8Basi hao walimwendea Filipo, mtu wa Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba, wakisema, Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu.

22Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.

23Naye Yesu akawajibu, akasema, Saa imefika atukuzwe Mwana wa Adamu.

24Rum 14:9; 1 Kor 15:36Amin, amin, nawaambia, Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.

25Mt 10:39; Lk 14:26; 17:33Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.

26Yn 14:3; 17:24Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.

Yesu Anena kuhusu Kifo chake

27 Zab 6:3; 42:5; Mt 26:38 Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.

28Yn 1:51; 5:37; Mt 3:17; 17:5Baba, ulitukuze jina lako. Basi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.

29Lk 22:43Basi mkutano uliosimama karibu wakasikia, walisema ya kwamba kumekuwa ngurumo; wengine walisema, Malaika amesema naye.

30Yn 11:42Yesu akajibu, akasema, Sauti hiyo haikuwako kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.

31Yn 14:30; 16:11; Lk 10:18Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo; sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.

32Yn 8:28Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.

33Aliyanena hayo akionyesha ni mauti gani atakayokufa.

34Zab 110:4; Isa 9:7; Dan 7:14Basi mkutano wakamjibu, Sisi tumesikia katika torati ya kwamba Kristo adumu hata milele; nawe wasemaje ya kwamba imempasa Mwana wa Adamu kuinuliwa? Huyu Mwana wa Adamu ni nani?

35Yn 8:12; 9:5; 11:10Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.

36Efe 5:8; Mt 23:39Maadamu mnayo nuru, iaminini nuru hiyo, ili mpate kuwa wana wa nuru.

Kutoamini kwa Watu

Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake, akajificha wasimwone.

37Walakini ajapokuwa amefanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, hawakumwamini;

38Isa 53:1; Rum 10:16ili litimie lile neno la nabii Isaya alilolisema,

Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu;

Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?

39 Isa 6:9,10; Mt 13:14,15 Ndiyo sababu wao hawakuweza kusadiki; kwa maana Isaya alisema tena,

40Amewapofusha macho,

Ameifanya mizito mioyo yao;

Wasije wakaona kwa macho yao,

Wakafahamu kwa mioyo yao,

Wakaongoka, nikawaponya.

41 Isa 6:1 Maneno hayo aliyasema Isaya, kwa kuwa aliuona utukufu wake, akataja habari zake.

42Yn 7:48; 9:22Walakini hata katika wakuu walikuwamo wengi waliomwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumkiri, wasije wakatengwa na sinagogi.

43Yn 5:44Kwa maana walipenda utukufu wa wanadamu kuliko utukufu wa Mungu.

44 Mt 10:40 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.

45Yn 14:9Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.

46Yn 8:12; 12:35Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

47Yn 3:17; 8:15; Lk 9:56Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

48Ebr 4:12; Ufu 19:15Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.

49Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.

50Yn 8:26,28Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help