Zab 79 - Swahili Union Version Bible

Ombi la Huruma kwa YerusalemuZaburi ya Asafu

1 2 Fal 25:8-10; 2 Nya 36:17-19; Yer 26:18; Yer 52:12-14 Ee Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,

Wamelinajisi hekalu lako takatifu.

Wamefanya Yerusalemu chungu chungu.

2 Yer 7:33 Wameziacha maiti za watumishi wako

Ziwe chakula cha ndege wa angani.

Na miili ya watauwa wako

Iwe chakula cha wanyama wa nchi.

3 Ufu 11:9 Wamemwaga damu yao kama maji

Pande zote za Yerusalemu,

Wala hapakuwa na mzishi.

4Tumekuwa lawama kwa jirani zetu,

Mzaha na dhihaka kwao wanaotuzunguka.

5 Kum 29:20; Eze 36:5 Ee BWANA, hata lini? Utaona hasira milele?

Wivu wako utawaka kama moto?

6 Isa 45:4; Zab 53:4 Ukali wako uwamwagie mataifa wasiokujua,

Na falme za hao wasioliitia jina lako.

7Kwa maana wamemla Yakobo,

Na matuo yake wameyaharibu.

8 Isa 43:25 Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu,

Rehema zako zije kutulaki hima,

Kwa maana tumedhilika sana.

9 Yos 7:0; Yer 14:7 Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,

Kwa ajili ya utukufu wa jina lako.

Utuokoe, utughofiri dhambi zetu,

Kwa ajili ya jina lako.

10Kwa nini mataifa kusema,

Yuko wapi Mungu wao?

Kisasi cha damu ya watumishi wako iliyomwagika

Kijulike kati ya mataifa machoni petu.

11 Hes 14:17 Kuugua kwake aliyefungwa

Na kuingie mbele zako.

Kwa kadiri ya uweza wa mkono wako

Uwahifadhi wana wa mauti.

12Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao

Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana.

13 Isa 43:21 Na sisi tulio watu wako,

Na kondoo za malisho yako,

Tutakushukuru milele;

Tutazisimulia sifa zako kizazi kwa kizazi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help