1
9 Hos 12:4 Mungu akamtokea Yakobo tena, aliporudi kutoka Padan-aramu akambariki.
10Mwa 17:5; 32:28Mungu akamwambia, Jina lako ni Yakobo; hutaitwa tena Yakobo, lakini Israeli litakuwa jina lako. Akamwita jina lake, Israeli.
11Mwa 17:4-8; 48:3,4; Kut 6:3Mungu akamwambia, Mimi ni Mungu Mwenyezi, uzidi ukaongezeke. Taifa na kundi la mataifa watatoka kwako, na wafalme watatoka viunoni mwako.
12Mwa 12:7; 13:15; 28:13; Kut 32:13Na nchi hii niliyowapa Ibrahimu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.
13Mwa 17:22Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.
14Mwa 28:18-19Yakobo akasimamisha nguzo mahali aliposema naye, nguzo ya mawe, akamimina juu yake sadaka ya kinywaji, akamimina mafuta juu yake.
15Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.
Kuzaliwa kwa Benyamini na Kufa kwa Raheli16Wakasafiri kutoka Betheli, hata ukabaki mwendo wa kitambo tu kufika Efrathi, Raheli akashikwa na utungu wa kuzaa, na utungu wake ulikuwa mzito.
17Mwa 30:24Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.
18Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
19Mwa 48:7; Rut 1:2; 4:11; Mik 5:2; Mt 2:6Akafa Raheli, akazikwa katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.
201 Sam 10:2Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.
21Mik 4:8Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi.
22Mwa 49:4; 1 Nya 5:1Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari.
Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
23Mwa 46:8; Kut 1:2Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
24Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.
25Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.
26Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Kufa kwa Isaka27 Mwa 13:18; Yos 14:15 Yakobo akaja kwa Isaka, babaye, huko Mamre, mji wa Arba, ndio Hebroni, walipokaa ugenini Ibrahimu na Isaka.
28Siku za Isaka zilikuwa miaka mia na themanini.
29Mhu 12:7; Mwa 15:15; 25:8,9; 49:31Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.