1 Kut 12:51 Haleluya.
Israeli alipotoka Misri,
Na Yakobo katika watu wa lugha ya kigeni.
2Yuda ilikuwa patakatifu pake,
Israeli milki yake.
3 Kut 14:21; Yos 3:16 Bahari iliona ikakimbia,
Yordani ilirudishwa nyuma.
4 Zab 29:6; 68:16; Hab 3:6 Milima iliruka kama kondoo waume,
Vilima kama wana-kondoo.
5Ee bahari, una nini, ukimbie?
Yordani, urudi nyuma?
6Enyi milima, mruke kama kondoo waume?
Enyi vilima, kama wana-kondoo?
7Tetemeka, Ee nchi, mbele za uso wa Bwana,
Mbele za uso wa Mungu wa Yakobo.
8 Kut 17:1-7; Hes 20:2-13; Zab 107:35 Augeuza mwamba kuwa ziwa la maji,
Jiwe gumu kuwa chemchemi.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.