Zab 121 - Swahili Union Version Bible

Hakikisho la Ulinzi wa MunguWimbo wa Upandaji Mlima.

1Nitayainua macho yangu niitazame milima,

Msaada wangu utatoka wapi?

2Msaada wangu u katika BWANA,

Aliyezifanya mbingu na nchi.

3 1 Sam 2:9; Isa 27:3 Asiuache mguu wako usogezwe;

Asisinzie akulindaye;

4Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi,

Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

5BWANA ndiye mlinzi wako;

BWANA ni uvuli mkono wako wa kuume.

6 Isa 49:10 Jua halitakupiga mchana,

Wala mwezi wakati wa usiku.

7 Ayu 5:19; Zab 91:9,10; Mit 12:21 BWANA atakulinda na mabaya yote,

Atakulinda nafsi yako.

8 Kum 28:6; Mit 2:8 BWANA atakulinda utokapo na uingiapo,

Tangu sasa na hata milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help