1 Kut 25:22 BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;
Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2BWANA katika Sayuni ni mkuu,
Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3 Kum 28:58; Isa 6:3; Ufu 4:8 Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa;
Ndiye mtakatifu.
4 Kum 32:3,4; Ayu 36:5; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Mwa 18:25 Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu;
Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili;
Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.
5 1 Nya 28:2; Zab 132:7; Isa 66:1 Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
6Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,
Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,
Walipomwita Bwana aliwaitikia;
7 Kut 19:9; Kut 33:9; Hes 12:5 Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8 Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20 Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
9Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana BWANA, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.