Zab 21 - Swahili Union Version Bible

Shukrani kwa UshindiKwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1Ee BWANA, mfalme atazifurahia nguvu zako,

Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana.

2 Yn 11:42 Umempa haja ya moyo wake,

Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.

3Maana umemsogezea baraka za heri,

Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

4 2 Sam 7:19 Alikuomba uhai, ukampa,

Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele.

5Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,

Heshima na adhama waweka juu yake.

6Maana umemfanya kuwa baraka za milele,

Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako.

7 Zab 91:2 Kwa kuwa mfalme humtumaini BWANA,

Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa.

8Mkono wako utawapata adui zako wote,

Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia.

9 Kum 32:22 Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto,

Wakati wa ghadhabu yako.

BWANA atawameza kwa ghadhabu yake,

Na moto utawala.

10Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi,

Na wazao wao katika wanadamu.

11Madhali walinuia kukutenda mabaya,

Waliwaza hila wasipate kuitimiza.

12Kwa maana utawafanya kukupa kisogo,

Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale.

13 Ufu 15:3,4 Ee BWANA, utukuzwe kwa nguvu zako,

Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help