Zab 3 - Swahili Union Version Bible

Mwamini Mungu katika DhikiZaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu.

1 2 Sam 15:13—17:22 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,

Ni wengi wanaonishambulia,

2 2 Sam 16:8; Zab 22:7,8 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,

Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3 2 Fal 25:27; Zab 27:6 Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4Kwa sauti yangu namwita BWANA

Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5 Zab 4:8; Mit 3:24; Mdo 12:6 Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka,

Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

6Sitayaogopa makumi elfu ya watu,

Waliojipanga juu yangu pande zote.

7BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,

Maana umewapiga taya adui zangu wote;

Umewavunja meno wasio haki.

8 Zab 37:39,40; Mit 21:31; Hes 13:4 Wokovu una BWANA;

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help