1 Mt 5:48; Kol 3:12 Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa;
2Kut 29:18; Zab 40:6; Gal 2:20; Ebr 10:10; Kol 3:13; Eze 20:41mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
Zikataeni Njia za Kipagani3 Efe 4:19; Kol 3:5 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
4Efe 4:29; Kol 3:8wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
51 Kor 6:9,10; Kol 3:5; Mdo 8:21Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6Rum 1:18; Kol 2:4,8Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.
7Basi msishirikiane nao.
8Efe 2:11,13; Lk 16:8; 1 Pet 2:9; Yn 12:36Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,
9kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;
10Rum 12:2mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.
11Yn 16:8Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;
12Rum 1:24kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.
13Yn 3:20,21Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.
14Isa 26:19; 60:1; Rum 13:11; 6:13Hivyo husema,
Amka, wewe usinziaye,
Ufufuke katika wafu,
Na Kristo atakuangaza.
15 Mt 10:16; Kol 4:5 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16Kol 4:5mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.
17Rum 12:2Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.
18Mit 23:31; Lk 21:34Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
19Kol 3:16-17; Zab 33:2,3mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20Kol 3:17na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
Nyumba ya Kikristo21 1 Pet 5:5 hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.
22 Kol 3:18; 1 Pet 3:1; Mwa 3:16 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
231 Kor 11:3; Kol 1:18Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Kol 3:19; 1 Pet 3:7 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
26Tit 3:5ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;
27Zab 45:13; 2 Kor 11:2apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
30Efe 1:23; 1 Kor 6:15; Mwa 2:23Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31Mwa 2:24Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
32Ufu 19:7Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.
33Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.