1Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
2Mt 18:6,7Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa.
3Mt 18:15Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
4Mt 18:21,22Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
5 Mk 9:24 Mitume wakamwambia Bwana, Tuongezee imani.
6Mt 17:20; 21:21Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii.
7Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula?
8Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa?
9Je! Atampa asante yule mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
10Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.
Yesu Awaponya watu kumi wenye Ukoma11 Lk 9:51; 13:22 Ikawa walipokuwa njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
12Law 13:45,46Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali,
13wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu!
14Law 13:49; 14:1-32; Lk 5:14Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
15Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu;
16akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi?
18Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu?
19Lk 7:50Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
Kuja kwa Ufalme20 Yn 18:36; 3:3 Na alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza;
21Mt 24:23; Yn 1:26; 12:35wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.
22Akawaambia wanafunzi, Siku zitakuja mtakapotamani kuona siku moja katika siku zake Mwana wa Adamu, msiione.
23Lk 21:8Tena watawaambia, Tazama, kule! Tazama, huku! Msiondoke mahali mlipo, wala msiwafuate;
24Mt 24:26,27kwa kuwa, kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hata upande huu chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.
25Lk 9:22Lakini kwanza, hana budi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi hiki.
26Mwa 6:5-8; Mt 24:37-39Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.
27Mwa 7:6-24Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.
28Mwa 18:20—19:25Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
29Mwa 19:24,25lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
30Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
31Mt 24:17-18; Mk 13:15-16; Mwa 19:26Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma.
32Mwa 19:26Mkumbukeni mkewe Lutu.
33Mt 10:39; 16:25; Mk 8:35; Lk 9:24; Yn 12:25Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza ataiponya.
34Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
35Mt 24:40,41Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja; mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
37Ayu 39:30; Mt 24:28Wakajibu, wakamwuliza, Wapi, Bwana? Akawaambia, Ulipo mzoga, ndipo watakapokutanika tai.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.