Zek 6 - Swahili Union Version Bible

Maono ya Nane: Magari Manne ya Vita

1Nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, yanatokea magari ya vita manne, yanatoka kati ya milima miwili, na milima hiyo ilikuwa ni milima ya shaba.

2Zek 1:8; Ufu 6:4,5Katika gari la kwanza walikuwa farasi wekundu; na katika gari la pili walikuwa farasi weusi;

3Ufu 6:2na katika gari la tatu walikuwa farasi weupe; na katika gari la nne walikuwa farasi wa rangi ya kijivujivu.

4Zek 5:10Nikajibu, nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Hawa ni nini, Bwana wangu?

5Zab 68:17; Ebr 1:7,14; 1 Fal 22:19; Ayu 1:6; Dan 7:10; Lk 1:19; Ufu 7:1Malaika akajibu, akaniambia, Hawa ni pepo nne za mbinguni, zitokeazo baada ya kusimama mbele za Bwana wa dunia yote.

6Yer 1:14Gari lile lenye farasi weusi latoka kwenda hata nchi ya kaskazini; nao farasi weupe wakatoka wakafuata nyuma yao; na wale wa rangi ya kijivujivu wakatoka kwenda hata nchi ya kusini.

7Mwa 13:17Na wale wekundu wakatoka, wakataka kwenda huko na huko katika dunia; naye akawaambia, Haya! Tokeni, mwende huko na huko katika dunia. Basi wakaenda huko na huko katika dunia.

8Mhu 10:4Ndipo akaniita, akaniambia akisema, Tazama, wale waendao mpaka nchi ya kaskazini wameituliza roho yangu katika nchi ya kaskazini.

Kutawazwa kwa Chipukizi

9Neno la BWANA likanijia, kusema,

10Ezr 2:1Pokea vitu mikononi mwa baadhi ya watu waliohamishwa, yaani, Heldai, na Tobia, na Yedaya; na siku iyo hiyo enenda ukaingie katika nyumba ya Yosia, mwana wa Sefania, waliyoifikia kutoka Babeli;

11Kut 28:36naam, pokea fedha na dhahabu, ukafanye taji, ukamvike kichwani Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu;

12Isa 9:6; 4:2; Mik 5:5; Mal 3:1; Yer 23:5; 33:15; Zek 13:7; 3:8; Mk 15:39; Lk 1:78; Yn 1:45; Zab 80:15-17; Mt 16:18; Efe 2:20; Flp 2:9; Ebr 2:9ukamwambie, ukisema, BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la BWANA.

13Zab 21:5; 110:4; Isa 22:24; Ebr 3:1Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.

14Mk 14:9Na hizo taji zitakuwa za Heldai, na Tobia, na Yedaya; na kwa fadhili za mwana wa Sefania; ziwe ukumbusho katika hekalu la BWANA.

15Efe 2:13Nao walio mbali watakuja na kujenga katika hekalu la BWANA, nanyi mtajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Na haya yatatokea, kama mkijitahidi kuitii sauti ya BWANA, Mungu wenu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help