Zab 53 - Swahili Union Version Bible

Kushutumiwa kwa Wasiomwamini MunguKwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Mahalathi. Utenzi wa Daudi.

1 Rum 3:10-12; Zab 10:4 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;

Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza,

Hakuna atendaye mema.

2 Zab 33:13; 2 Nya 15:2 Toka mbinguni MUNGU aliwachungulia wanadamu,

Aone kama yuko mtu mwenye akili,

Amtafutaye Mungu.

3 Mhu 7:29 Kila mtu amepotoka, wameoza wote pamoja,

Hakuna atendaye mema,

La! Hata mmoja.

4 Yer 4:22 Je! Wafanyao maovu hawajui?

Walao watu wangu kama walavyo mkate,

Hawakumwita MUNGU.

5Hapo waliingiwa na hofu pasipokuwapo hofu,

Maana Mungu ameitawanya mifupa yake aliyekuhusuru.

Umewatia aibu,

Kwa sababu MUNGU amewadharau.

6Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!

MUNGU awarudishapo wafungwa wa watu wake;

Yakobo atashangilia,

Israeli atafurahi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help