Zab 7 - Swahili Union Version Bible

Ombi la Msaada dhidi ya WatesajiOmbolezo la Daudi, aliloimba kwa BWANA kuhusu Kushi, Mbenyamini.

1BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe,

Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.

2 1 Pet 5:8 Asije akaipapura nafsi yangu kama simba,

Akiivunja-vunja pasipokuwa na wa kuponya.

3 2 Sam 16:7 BWANA, Mungu wangu, ikiwa nimetenda haya,

Ikiwa mna uovu mikononi mwangu,

4 1 Sam 24:7 Ikiwa nimemlipa mabaya

Yeye aliyekaa kwangu salama;

(Hasha! Nimemponya yeye

Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)

5Basi adui na anifuatie,

Na kuikamata nafsi yangu;

Naam, aukanyage uzima wangu,

Na kuulaza utukufu wangu mavumbini.

6 Zab 94:2 BWANA uondoke kwa hasira yako;

Ujiinue juu ya jeuri ya watesi wangu;

Uamke kwa ajili yangu;

Umeamuru hukumu.

7Kusanyiko la mataifa na likuzunguke,

Na juu yake uketi utawale.

8BWANA atawaamua mataifa,

BWANA, unihukumu mimi,

Kwa kadiri ya haki yangu,

Sawasawa na unyofu nilio nao.

9 Ufu 2:23; 1 Sam 16:7 Ubaya wao wasio haki na ukome,

Lakini umthibitishe mwenye haki.

Kwa maana mjaribu mioyo na viuno

Ndiye Mungu aliye mwenye haki.

10Ngao yangu ina Mungu,

Awaokoaye wanyofu wa moyo.

11Mungu ni mwamuzi mwenye haki,

Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku.

12Mtu asiporejea ataunoa upanga wake;

Ameupinda uta wake na kuuweka tayari;

13Naye amemtengenezea silaha za kufisha,

Akifanya mishale yake kuwa ya moto.

14Tazama, huyu ana utungu wa uovu,

Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.

15 Est 7:10; Mit 5:22 Amechimba shimo, amelichimba chini sana,

Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!

16 1 Fal 2:32 Madhara yake yatamrejea kichwani pake,

Na dhuluma yake itamshukia utosini.

17Nitamshukuru BWANA kwa kadiri ya haki yake;

Nitaliimbia jina la BWANA aliye juu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help