Lk 21 - Swahili Union Version Bible

Sadaka ya Mjane

1 Mk 12:41-44 Akainua macho yake akawaona matajiri wakitia sadaka zao katika sanduku la hazina.

2Akamwona mjane mmoja maskini akitia mle senti mbili.

32 Kor 8:12Akasema, Hakika nawaambia, huyu mjane maskini ametia zaidi kuliko wote;

4maana, hao wote walitia sadakani katika mali iliyowazidi, bali huyu katika umaskini wake ametia vyote alivyokuwa navyo.

Kuangamizwa kwa Hekalu Kwatabiriwa

5 Mt 24:1-21; Mk 13:1-19 Na watu kadha wa kadha walipokuwa wakiongea habari za hekalu, jinsi lilivyopambwa kwa mawe mazuri na sadaka za watu, alisema,

6Lk 19:44Haya mnayoyatazama, siku zitakuja ambapo halitasalia jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa.

Ishara na Mateso

7Wakamwuliza wakisema, Mwalimu, mambo hayo yatakuwa lini? Nayo ni nini ishara ya kuwa mambo hayo ya karibu kutukia?

8Dan 7:22Akasema, Angalieni, msije mkadanganyika, kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ndiye; tena, Majira yamekaribia. Basi msiwafuate hao.

9Dan 2:28Nanyi mtakaposikia habari za vita na fitina, msitishwe; maana, hayo hayana budi kutukia kwanza, lakini ule mwisho hauji upesi.

10 Isa 19:2; 2 Nya 15:6 Kisha aliwaambia, Taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme;

11kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi; na njaa na tauni mahali mahali; na mambo ya kutisha na ishara kuu kutoka mbinguni.

12Lk 12:11Lakini, kabla hayo yote hayajatokea, watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi, na kuwaua magerezani, mkipelekwa mbele ya wafalme na maliwali kwa ajili ya jina langu.

13Na hayo yatakuwa ushuhuda kwenu.

14Lk 12:11-12

Mt 10:19Basi, kusudieni mioyoni mwenu, kutofikiri-fikiri kwanza mtakavyojibu;

15Mdo 6:10kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

16Nanyi mtasalitiwa na wazazi wenu, na ndugu zenu, na jamaa zenu, na rafiki zenu, nao watawafisha baadhi yenu.

17Mt 10:21,22Nanyi mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.

18Lk 12:7; 1 Sam 14:45Walakini hautapotea hata unywele mmoja wa vichwa vyenu.

192 Nya 15:7; Ebr 10:36Nanyi kwa subira yenu mtaziponya nafsi zenu.

Unabii wa kuangamizwa kwa Yerusalemu

20Lakini, hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia.

21Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.

22Hos 9:7; Kum 32:35; Yer 5:29Kwa kuwa siku hizo ndizo za mapatilizo, ili yatimizwe yote yaliyoandikwa.

231 Kor 7:26Ole wao wenye mimba na wanaonyonyesha katika siku hizo! Kwa kuwa kutakuwa na shida nyingi katika nchi, na hasira juu ya taifa hili.

24Kum 28:64; Zek 12:3; Isa 63:18; Zab 79:1; Dan 8:10; Rum 11:25; Ufu 11:2Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hata majira ya Mataifa yatakapotimia.

Kuja kwa Mwana wa Mtu

25 Mt 24:29,30; Mk 13:24-26 Isa 13:10; Eze 32:7; Yoe 2:31; Ufu 6:12-13; Zab 65:7 Tena, kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota; na katika nchi dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake;

26Isa 34:4watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayoupata ulimwengu. Kwa kuwa nguvu za mbinguni zitatikisika.

27Dan 7:13; Ufu 1:7; Mt 26:64Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingi.

28Flp 4:4,5Basi mambo hayo yaanzapo kutokea, changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.

Funzo la Mtini

29 Mt 24:32-35; Mk 13:28-31 Akawaambia mfano; Utazameni mtini na miti mingine yote.

30Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekwisha kuwa karibu.

31Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.

32Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote yatimie.

33Lk 16:17Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

Himizo za kuwa Waangalifu

34 Lk 17:27; Mk 4:19; Mt 24:49 Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;

35Isa 24:17; 1 The 5:3kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.

36Mk 13:33; Ufu 6:17Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.

37 Lk 19:47; Yn 8:1 Basi, kila mchana alikuwa akifundisha hekaluni, na usiku huenda kulala katika mlima uitwao wa Mizeituni.

38Na watu wote walikuwa wakiamka mapema waende hekaluni ili kumsikiliza.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help