1 atakunywa baada yao.
27Hab 2:16Nawe utawaambia hivi, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu.
28Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.
29Mit 11:31; Yer 49:12; Oba 1:16; Lk 23:31; 1 Pet 4:17; Eze 38:21Maana angalieni, ninaanza kutenda mabaya katika mji uitwao kwa jina langu, je! Mtaachiliwa ninyi msiadhibiwe? Hamtaachiliwa msiadhibiwe; kwa maana nitauita upanga ule uwapige wote wakaao katika dunia, asema BWANA wa majeshi.
30Isa 42:13; Yoe 3:16; Amo 1:2; Zab 68:16Basi, tabiri wewe maneno haya yote juu yao, na kuwaambia,
BWANA atanguruma toka juu,
Naye atatoa sauti yake toka patakatifu pake;
Atanguruma sana juu ya zizi lake;
Atapiga kelele kama mtu akanyagaye zabibu,
Juu ya wenyeji wote wa dunia.
31 Hos 4:1; Mik 6:2; Yoe 3:2 Mshindo utafika hata mwisho wa dunia;
Maana BWANA ana mashindano na mataifa,
Atateta na watu wote wenye mwili;
Na waovu atawatoa wauawe kwa upanga; asema BWANA.
32BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
33Isa 34:2-8; Yer 12:12; Ufu 19:17-21Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.
34Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
35Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.
36Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao.
37Zab 97:1-3; Isa 66:15; Ebr 12:29Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA.
38Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.