Zab 47 - Swahili Union Version Bible

Utawala wa Mungu juu ya MataifaKwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.

1Enyi watu wote, pigeni makofi,

Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.

2 Kum 7:21; Neh 1:5; Mal 1:14 Kwa kuwa BWANA Aliye juu, mwenye kuogofya,

Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.

3 Zab 18:47 Atawatiisha watu wa nchi chini yetu,

Na mataifa chini ya miguu yetu.

4 1 Pet 1:4 Atatuchagulia urithi wetu,

Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.

5 Zab 24:7-10; Mdo 1:9; Efe 4:8-10; 1 Tim 3:16 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

BWANA kwa sauti ya baragumu.

6Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;

Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.

7 Zek 14:9; 1 Kor 14:15 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa akili.

8Mungu awamiliki mataifa,

Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.

9Wakuu wa watu wamekusanyika,

Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu.

Maana ngao za dunia zina Mungu,

Ametukuka sana.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help