1 1 Nya 16:34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 118:1; Yer 33:11 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Kut 18:11; Kum 10:17 Mshukuruni Mungu wa miungu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 1 Tim 6:15; Ufu 17:14 Mshukuruni Bwana wa mabwana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4Yeye peke yake afanya maajabu makuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 Mwa 1:1; Mit 3:19 Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 Mwa 1:2; Yer 10:12 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 Mwa 1:16; Kum 4:19 Yeye aliyefanya mianga mikubwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8Jua litawale mchana;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9Mwezi na nyota zitawale usiku;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10 Kut 12:29 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 Kut 12:51 Akawatoa Waisraeli katikati yao;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 Zab 78:13; Kut 14:21-29 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14Akawavusha Israeli katikati yake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 Kum 8:15 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18 Kum 29:7 Akawaua wafalme mashuhuri;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19 Hes 21:21-30 Sihoni, mfalme wa Waamori;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20 Hes 21:31-35 Na Ogu, mfalme wa Bashani;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21 Yos 12:1 Akaitoa nchi yao iwe urithi;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22Urithi wa Israeli mtumishi wake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23 Mwa 8:1; Kum 32:36; Zab 102:17; Isa 63:9; Lk 1:48 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24Akatuokoa na watesi wetu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25 Zab 104:27 Kila chenye mwili akipa chakula chake;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26Mshukuruni Mungu wa mbingu;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.