1 Ebr 1:1; 2 Pet 1:21 Neno la BWANA lililomjia Yoeli, mwana wa Pethueli.
2 Kum 4:32; Isa 7:17; Dan 12:1; Yoe 2:2; Mt 24:21 Sikieni haya, enyi wazee;
Sikilizeni, enyi wenyeji wote wa nchi.
Je! Mambo haya yamekuwako katika siku zenu,
Au katika siku za baba zenu?
3 Zab 78:4 Waarifuni watoto wenu habari yake,
Watoto wenu wakawaambie watoto wao,
Na watoto wao wakakiambie kizazi kingine.
4Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
5 Isa 32:10 Levukeni, enyi walevi, mkalie;
Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;
Kwa sababu ya divai mpya;
Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
6 Mit 30:25; Ufu 9:8 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,
Lenye nguvu, tena halina hesabu;
Meno yake ni kama meno ya simba,
Naye ana magego ya simba mkubwa.
7 Isa 5:6 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8 Isa 22:12; Mit 2:17 Ombolea kama mwanamwali avaaye magunia
Kwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 Yoe 2:14 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji
Zimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;
Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.
10 Yer 12:11; Isa 24:7 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
11 Yer 14:3 Tahayarini, enyi wakulima;
Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu;
Kwa ajili ya ngano na shayiri,
Maana mavuno ya mashamba yamepotea.
12 Isa 9:3; Yer 48:33; Hos 9:1,2 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia;
Nao mkomamanga na mtende na mtofaa;
Naam, miti yote ya mashamba imekauka;
Maana furaha imekauka katika wanadamu.
Mwito wa Toba na Sala13 Yer 4:8 Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani;
Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu;
Njoni mlale usiku kucha katika magunia,
Enyi wahudumu wa Mungu wangu;
Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji
Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu.
14 2 Nya 20:3,13 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini,
Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi;
Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu,
Na kumlilia BWANA,
15 Yer 30:7; Yoe 2:3; Amo 5:16-18; Isa 13:6 Ole wake siku hii!
Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
16Kum 12:7,12; 16:11Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?
17Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
181 Fal 18:5; Hos 4:3Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
19Ee BWANA, nakulilia wewe;
Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,
Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.
20 Ayu 38:41; Zab 104:31; 1 Fal 17:7 Naam, wanyama wa mashamba wanakutwetea wewe;
Kwa maana vijito vya maji vimekauka,
Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.