1 Mk 1:40-44; Lk 5:12-14 Naye aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata.
2Na tazama, akaja mtu mwenye ukoma akamsujudia, akisema, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.
3Yesu akanyosha mkono, akamgusa, akisema Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukatakasika.
4Law 13:49; 14:1-32; Mt 9:30; Mk 7:36; Lk 17:14Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; ila enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, ukaitoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
Yesu Amponya Mtumishi wa Afisa5 Lk 7:1-10 Yn 4:47 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.
8Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.
9Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
10Mt 15:28Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.
11Lk 13:29; Isa 49:12; 59:19; Mal 1:11; Zab 107:3Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
12Mt 22:13; 24:51; 25:30; Lk 13:28bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
13Mt 9:29; 15:28Naye Yesu akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake akapona saa ile ile.
Yesu Aponya Wengi Nyumbani kwa Petro14 Mk 1:29-34; Lk 4:38-41 1 Kor 9:5 Hata Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani hawezi homa.
15Akamgusa mkono, homa ikamwacha; naye akaondoka, akawatumikia.
16Hata kulipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo; akawatoa pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,
17Isa 53:4ili litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
Mwenyewe aliutwaa udhaifu wetu,
Na kuyachukua magonjwa yetu.
Watakaokuwa Wafuasi wa Yesu18 Mk 4:35; Lk 8:22 Naye Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng’ambo.
19Lk 9:57-60Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako.
202 Kor 8:9Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
211 Fal 19:20Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu.
22Yn 1:43; 5:25; Rum 6:13Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.
Yesu Atuliza Dhoruba23 Mk 4:36-41; Lk 8:23-25 Zab 4:8 Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata.
24Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi.
25Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.
26Mt 14:31; 16:8Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu.
27Wale watu wakamaka wakisema, Huyu ni mtu wa namna gani hata pepo na bahari zamtii?
Yesu Awaponya Wagadara Wenye Pepo28 Mk 5:1-17; Lk 8:26-37 Naye alipofika ng’ambo, katika nchi ya Wagerasi, watu wawili wenye pepo walikutana naye, wanatoka makaburini, wakali mno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile.
29Lk 4:41; 2 Pet 2:4Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu?
30Basi, kulikuwako mbali nao kundi la nguruwe wengi wakilisha.
31Wale pepo wakamsihi, wakisema, Ukitutoa, tuache twende, tukaingie katika lile kundi la nguruwe.
32Akawaambia, Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika nguruwe; na kumbe! Kundi lote wakatelemka kwa kasi gengeni hata baharini, wakafa majini.
33Lakini wachungaji walikimbia, wakaenda zao mjini, wakazieneza habari zote na habari za wale wenye pepo pia.
34Na tazama, mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; nao walipomwona, walimsihi aondoke mipakani mwao.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.