1 Eze 23:3; Hos 2:15 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Israeli na aseme sasa,
2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Lakini hawakuniweza.
3 Ebr 11:36 Wakulima wamelima mgongoni mwangu,
Wamefanya mirefu mifuo yao.
4 2 The 1:6 BWANA ndiye mwenye haki,
Amezikata kamba zao wasio haki.
5Na waaibishwe, warudishwe nyuma,
Wote wanaoichukia Sayuni.
6 Zab 37:2; Yer 17:5-6 Na wawe kama majani ya darini
Yanyaukayo kabla hayajamea.
7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,
Wala mfunga miganda kifua chake.
8 Rut 2:4; Zab 118:26 Wala hawasemi wapitao, Amani ya BWANA ikae nanyi,
Twawabariki kwa jina la BWANA.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.