Zab 122 - Swahili Union Version Bible

Wimbo wa Sifa na Sala kwa YerusalemuWimbo wa kupanda mlima.

1 Isa 2:3; Yer 31:6; Zek 8:21 Nalifurahi waliponiambia,

Na twende nyumbani kwa BWANA.

2Miguu yetu imesimama

Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.

3 2 Sam 5:9; Efe 2:21 Ee Yerusalemu uliyejengwa

Kama mji ulioshikamana,

4 Kum 16:16; Kut 16:34 Huko ndiko walikopanda kabila,

Kabila za BWANA;

Ushuhuda kwa Israeli,

Walishukuru jina la BWANA.

5Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,

Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.

6 Isa 62:6; Yer 51:50 Utakieni Yerusalemu amani;

Na wafanikiwe wakupendao;

7Amani na ikae ndani ya kuta zako,

Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.

8Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu

Niseme sasa, Amani ikae nawe.

9Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu,

Nikutafutie mema.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help