1 2 The 3:6 Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana.
2Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
31 The 5:23; Ebr 10:10; 1 Pet 1:16Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati;
41 Kor 6:13,15kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;
5Yer 10:25; Zab 79:6si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
6Zab 94:2Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosa katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana.
72 The 2:13,14Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso.
8Lk 10:16; Eze 36:27; 37:14Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
9 Yn 13:34; Yer 31:33,34 Katika habari ya upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
102 The 3:4Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini twawasihi, ndugu, mzidi sana.
11Efe 4:28; 2 The 3:8,12Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza;
12Kol 4:5; 1 Kor 5:12,13ili mwenende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu cho chote.
Kuja kwa Bwana13 1 Kor 15:20; Efe 2:12 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
14Rum 14:9; 1 Kor 15:3,4,12Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
151 Kor 15:51-52; 7:10,25Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti.
161 Kor 15:52; 2 The 1:7Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza.
17Yn 12:26; 17:24Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
18Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.