Zab 71 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Ulinzi wa Daima na Msaada

1Nimekukimbilia Wewe, BWANA,

Nisiaibike milele.

2Kwa haki yako uniponye, uniopoe,

Unitegee sikio lako, uniokoe.

3 Zab 44:4 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,

Nitakakokwenda sikuzote.

Umeamuru niokolewe,

Ndiwe genge langu na ngome yangu.

4Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi,

Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,

5 Yer 17:7; Rum 15:13 Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU,

Tumaini langu tokea ujana wangu.

6 Zab 22:9; Isa 46:3; Yer 3:4 Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,

Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,

Ninakusifu Wewe daima.

7 Isa 8:18; Zek 3:8; 1 Kor 4:9 Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi,

Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.

8Kinywa changu kitajazwa sifa zako,

Na heshima yako mchana kutwa.

9Usinitupe wakati wa uzee,

Nguvu zangu zipungukapo usiniache.

10 2 Sam 17:1; Mt 27:1 Kwa maana adui zangu wananiamba,

Nao wanaoniotea roho yangu hushauriana.

11Wakisema, Mungu amemwacha,

Mfuatieni, mkamateni, hakuna wa kumponya.

12 Zab 22:11; 35:22; 70:1 Ee Mungu, usiwe mbali nami;

Ee Mungu wangu, fanya haraka kunisaidia.

13 Zab 35:4; 40:14 Waaibishwe, watoweshwe, adui za nafsi yangu.

Wavikwe laumu na aibu wanaonitakia mabaya.

14Nami nitatumaini daima,

Nitazidi kuongeza sifa zake zote.

15 Zab 35:28; 40:5 Kinywa changu kitasimulia haki na wokovu wako

Mchana kutwa; maana sijui hesabu yake.

16 Zek 10:12; Efe 3:16; Flp 4:13; 2 Tim 2:1 Nitakuja na mambo ya ajabu ya Bwana MUNGU;

Nitawakumbusha watu haki yako Wewe peke yako.

17Ee Mungu, umenifundisha tokea ujana wangu;

Nimekuwa nikitangaza miujiza yako hata leo.

18Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi,

Ee Mungu, usiniache.

Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako,

Na kila atakayekuja uweza wako.

19 Zab 57:10; Mit 24:7; Isa 5:16; Kut 15:11; Zab 35:10; Isa 40:18,25 Na haki yako, Ee Mungu,

Imefika juu sana.

Wewe uliyefanya mambo makuu;

Ee Mungu, ni nani aliye kama Wewe?

20 Zab 60:3; Hos 6:1 Wewe, uliyetuonyesha mateso mengi, mabaya,

Utatuhuisha tena.

Utatupandisha juu tena

Tokea pande za chini ya nchi.

21Laiti ungeniongezea ukuu!

Urejee tena na kunifariji moyo.

22 2 Fal 19:22; Isa 60:9 Nami nitakushukuru kwa kinanda,

Na kweli yako, Ee Mungu wangu.

Nitakuimbia Wewe kwa kinubi,

Ee Mtakatifu wa Israeli.

23 Zab 103:4 Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo,

Na nafsi yangu uliyoikomboa.

24Ulimi wangu nao utasimulia

Haki yako mchana kutwa.

Kwa maana wameaibishwa,

Wametahayarika, wanaonitakia mabaya.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help