1Katika Yuda Mungu amejulikana,
Katika Israeli jina lake ni kuu.
2Kibanda chake pia kiko Salemu,
Na maskani yake iko Sayuni.
3 Zab 46:9; Eze 39:9 Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta,
Ngao, na upanga, na zana za vita.
4 Eze 38:12 Wewe U mwenye fahari na adhama,
Toka milima ya mateka.
5 Isa 46:12; Zab 13:3; Yer 51:39 Wametekwa wenye moyo thabiti;
Wamelala usingizi;
Wala hawakuiona mikono yao
Watu wote walio hodari.
6 Kut 15:1; Nah 2:13; Zek 12:4 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,
Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7 Ayu 41:10; Nah 1:6 Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe;
Naye ni nani awezaye kusimama ufanyapo hasira?
8Toka mbinguni ulitangaza hukumu;
Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9Mungu aliposimama ili kuhukumu
Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10 Kut 9:16 Maana hasira ya binadamu itakusifu,
Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11 Mhu 5:4; Zab 68:29 Wekeni nadhiri, mkaziondoe
Kwa BWANA, Mungu wenu.
Wote wanaomzunguka wamletee hedaya,
Yeye astahiliye kuogopwa.
12 Zab 68:35 Yeye huzikata roho za wakuu;
Na kuwatisha wafalme wa dunia.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.