2 The 3 - Swahili Union Version Bible

Hitaji la Maombi

1 Kol 4:3; 1 The 5:25 Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;

2tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na imani.

31 The 5:24Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.

41 The 4:10; Gal 5:10; 2 Kor 7:16Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tulivyowaagiza, tena kwamba mtayafanya.

5Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

Onyo juu ya Kutofanya Kazi

6 Mt 18:17; Rum 16:17; 1 The 5:14; 4:1 Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.

71 The 2:1; 1:6Mwajua wenyewe jinsi iwapasavyo kutufuata; kwa sababu hatukuenda bila utaratibu kwenu;

81 Kor 4:12; Flp 3:17; 1 The 2:9wala hatukula chakula kwa mtu ye yote bure; bali kwa taabu na masumbufu, usiku na mchana tulitenda kazi, ili tusimlemee mtu wa kwenu awaye yote.

9Mt 10:10; 1 Kor 4:16; 1 The 1:6,7Si kwamba hatuna amri, lakini makusudi tufanye nafsi zetu kuwa kielelezo kwenu, mtufuate.

10Mwa 3:19; 1 The 3:4; 4:11Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

111 The 5:14Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.

121 The 4:11Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

13Gal 6:9Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.

141 Kor 5:9,11Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;

151 The 5:13,14lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.

Salamu za Mwisho na Baraka

16 1 The 5:23 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote.

17 1 Kor 16:21 Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu.

18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help