Zab 50 - Swahili Union Version Bible

Ibada ya KweliZaburi ya Asafu.

1Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi,

Toka maawio ya jua hata machweo yake.

2Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,

Mungu amemulika.

3Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza,

Moto utakula mbele zake,

na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.

4 Mik 6:1,2 Ataziita mbingu zilizo juu,

Na nchi pia awahukumu watu wake.

5 Isa 13:3; 1 Kor 6:2; 1 The 3:13; Yud 1:14; Kut 24:7; Isa 59:20,21; Ebr 8:6 Nikusanyieni wacha Mungu wangu

Waliofanya agano nami kwa dhabihu.

6Na mbingu zitatangaza haki yake,

Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.

7Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,

Mimi nitakushuhudia, Israeli;

Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako.

8Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,

Na kafara zako ziko mbele zangu daima.

9 Isa 43:23; Mik 6:6; Mdo 17:25 Sitatwaa ng’ombe katika nyumba yako,

Wala beberu katika mazizi yako.

10Maana kila hayawani ni wangu,

Na makundi juu ya milima elfu.

11Nawajua ndege wote wa milima,

Na wanyama wote wa mashamba ni wangu

12Kama ningekuwa na njaa singekuambia,

Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo.

13Je! Nile nyama ya mafahali!

Au ninywe damu ya mbuzi!

14 Hes 14:2 Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;

Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.

15 Ayu 22:27; Zab 22:23; Mt 5:16; Yn 15:8 Ukaniite siku ya mateso;

Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.

16Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,

Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,

Na kuliweka agano langu kinywani mwako?

17 Mit 1:7; 5:12,13; Rum 2:21; 2 The 2:10-12 Maana wewe umechukia maonyo,

Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

18 Rum 1:32 Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,

Ukashirikiana na wazinzi.

19Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,

Na ulimi wako watunga hila.

20Umekaa na kumsengenya ndugu yako,

Na mwana wa mama yako umemsingizia.

21 Mhu 8:11; Rum 2:4 Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;

Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.

Walakini nitakukemea;

Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.

22Yafahamuni hayo,

Ninyi mnaomsahau Mungu,

Nisije nikawararueni,

Asipatikane mwenye kuwaponya.

23Atoaye dhabihu za kushukuru,

Ndiye anayenitukuza.

Naye autengenezaye mwenendo wake,

Nitamwonyesha wokovu wa Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help