Kut 31 - Swahili Union Version Bible

Bezaleli na Oholiabu

1BWANA akanena na Musa, na kumwambia,

2Kut 35:30; 1 Nya 2:20Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;

3Kut 35:31; 1 Fal 7:14; Isa 28:26; 1 Kor 12:4-8nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,

4ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,

5na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

6Kut 35:34; 28:3; 36:1Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;

7Kut 36:8yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;

8na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba;

9na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake;

10na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani;

11na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

Sheria za Sabato

12BWANA akasema na Musa, na kumwambia,

13Law 19:3; 26:2; Eze 20:12; 44:24Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.

14Neh 9:14; Kum 5:12; Isa 56:6; 58:13; Eze 20:12; Kut 35:2; Hes 15:35Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

15Mwa 2:2; Kut 16:23; 20:8-11; 23:12; 28:36; 34:21; 35:2; Law 23:3; Kum 5:12-14Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa.

16Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.

17Kut 20:11; Eze 20:12; Mwa 1:31Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

Mbao mbili za Mawe ni Ushuhuda wa Agano

18 Kut 24:12; 32:15; 34:28,29; Kum 4:13; 5:22; 9:10,11; 2 Kor 3:3 Hapo BWANA alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help