Isa 48 - Swahili Union Version Bible

Mungu Muumbaji na Mkombozi

1 Kum 6:13; Yer 7:9; Sef 1:5 Sikieni haya, enyi watu wa nyumba ya Yakobo, mnaoitwa kwa jina la Israeli, mliotoka katika maji ya Yuda; mnaoapa kwa jina la BWANA, na kumtaja Mungu wa Israeli, lakini si kwa kweli, wala si kwa haki.

2Mik 3:11; Rum 2:17Maana hujiita wenyeji wa mji mtakatifu, hujitegemeza juu ya Mungu wa Israeli; BWANA wa majeshi ni jina lake.

3Yos 21:45Mimi nimehubiri mambo ya kale tangu zamani; naam, yalitoka katika kinywa changu, nikayadhihirisha; naliyatenda kwa ghafula, yakatokea.

4Kut 32:9; Kum 31:27Kwa sababu nalijua ya kuwa wewe u mkaidi, na shingo yako ni shingo ya chuma, na kipaji cha uso wako ni shaba;

5basi nimekuonyesha tangu zamani; kabla hayajatukia nalikuonyesha; usije ukasema, Sanamu yangu imetenda haya; sanamu yangu ya kuchonga, na sanamu yangu ya kuyeyusha, imeyaamuru.

6Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonyesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.

7Yameumbwa sasa, wala si tokea zamani; na kabla ya siku hii ya leo hukusikia habari yake; usije ukasema, Tazama, naliyajua.

8Zab 58:3Naam, hukusikia; naam, hukujua; naam, tokea zamani sikio lako halikuzibuka; maana nalijua ya kuwa wewe watenda kwa hila nyingi, nawe umeitwa mkosaji tangu kuzaliwa kwako;

9Yos 7:9; Zab 106:8kwa ajili ya jina langu nitaahirisha hasira yangu, na kwa ajili yako nitajizuia, ili nisifiwe, wala nisikukatilie mbali.

10Zab 66:10; Isa 1:25; Mal 3:3Tazama, nimekusafisha, lakini si kama fedha; nimekuchagua katika tanuru ya mateso.

11Kum 32:26; Isa 42:8Kwa ajili ya nafsi yangu, kwa ajili ya nafsi yangu, nitatenda haya; je! Litiwe unajisi jina langu? Wala sitampa mwingine utukufu wangu.

12 Kum 32:39; Isa 44:6; Ufu 1:17; 22:13 Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.

13Zab 102:25Naam, mkono wangu umeuweka msingi wa dunia, na mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu; niziitapo husimama pamoja.

14Kusanyikeni, ninyi nyote, mkasikie; ni nani miongoni mwao aliyehubiri haya? BWANA amempenda; atatimiza mapenzi yake juu ya Babeli, na mkono wake utakuwa juu ya Wakaldayo.

15Mimi, naam, mimi, nimenena; naam, nimemwita; nimemleta, naye ataifanikisha njia yake.

16Zek 2:8,9Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake.

17Zab 32:8BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

18Kum 5:29; Zab 81:13Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;

19Mwa 22:17; Hos 1:10Tena wazao wako wangalikuwa kama mchanga, na hao waliotoka katika tumbo lako kama chembe zake; jina lake lisingalikatika, wala kufutwa mbele zangu.

20 Zek 2:6,7; Kut 19:4; Ufu 18:4 Haya, tokeni katika Babeli,

Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo;

Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya,

Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni,

BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.

21 Hes 20:11; Neh 9:15; Zab 105:41; Isa 48:21; 1 Kor 10:4 Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani;

Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao;

Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.

22 Isa 57:21 Hapana amani kwa wabaya, asema BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help