Ayu 8 - Swahili Union Version Bible

Bildadi Anena: Ayubu Astahili Kutubu

1Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,

2Wewe utanena maneno haya hata lini?

Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?

3 Mwa 18:25; Kum 32:4; Ayu 34:12; Dan 9:14 Je! Mungu hupotosha hukumu?

Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?

4Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,

Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;

5Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,

Na kumsihi huyo Mwenyezi;

6Ukiwa wewe u safi na mwelekevu;

Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako,

Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.

7Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo,

Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.

8 Kum 4:32 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,

Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

9 Mwa 47:9; Zab 39:5 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,

Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)

10Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,

Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?

11Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope

Na makangaga kumea pasipo maji?

12 Zab 129:6; Yer 17:6; Yak 1:10,11; 1 Pet 1:24 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa,

Hunyauka mbele ya majani mengine.

13 Ayu 11:20; 18:14; Zab 112:10; Mit 10:28; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1,2 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;

Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;

14Uthabiti wake utavunjika,

Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.

15 Ayu 27:18 Ataitegemea nyumba yake, isisimame;

Atashikamana nayo, isidumu.

16Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,

Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.

17Mizizi yake huzonga-zonga chuguu,

Huangalia mahali penye mawe.

18 Ayu 7:10; Zab 37:36 Lakini, aking’olewa mahali pake,

Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.

19 Zab 113:7 Tazama, furaha ya njia yake ni hii,

Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.

20 Zab 37:24; 1 The 5:23,24 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu,

Wala hatawathibitisha watendao uovu.

21Bado atakijaza kinywa chako kicheko,

Na midomo yako ataijaza shangwe.

22Hao wakuchukiao watavikwa aibu;

Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help