1 Mwa 48:10; 1 Sam 3:2; Mhu 12:3 Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.
2Mit 27:1; Yak 4:14Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu.
3Mwa 25:27,28Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo;
4Mwa 48:9,15; 49:28; Kum 33:1; Ebr 11:20ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa.
5Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete.
6Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, akisema, Angalia, nimemsikia baba yako akisema na Esau, ndugu yako, akinena,
7Niletee mawindo, ukanifanyie chakula kitamu ili nile, na kukubariki mbele za BWANA kabla ya kufa kwangu.
8Mwa 27:13Basi, mwanangu, sikiliza sauti yangu kama nitakavyokuagiza.
9Enenda sasa kundini ukanitwalie wana-mbuzi wawili walio wema, nami nitawafanya chakula kitamu kwa baba yako, namna ile aipendayo.
10Mwa 48:15Kisha utampelekea baba yako, apate kula, ili akubariki kabla ya kufa kwake.
11 Mwa 25:25 Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.
12Mwa 27:22; 9:25; Kum 27:18Labda baba yangu atanipapasa, nami nitakuwa machoni pake kama mdanganyifu; nami nitaleta juu yangu laana wala si mbaraka.
13Mwa 43:9; 1 Sam 25:24; 2 Sam 14:9; Mt 27:25Mamaye akamwambia, Laana yako na iwe juu yangu, mwanangu, usikie sauti yangu tu, enenda ukaniletee wana-mbuzi.
14Mwa 27:4,9Akaenda, akawatwaa, akamletea mamaye. Mamaye akafanya chakula kitamu namna ile aliyopenda babaye.
15Mwa 27:27Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.
16Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake.
17Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu, na mkate alioufanya.
18Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu?
191 Fal 13:18; 14:2; Isa 28:15; Zek 13:4Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondoka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki.
20Kut 20:7Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha.
21Mwa 27:12Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo.
22Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau.
23Mwa 27:16Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki.
24Rum 3:7,8; Efe 4:25Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi.
25Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogezea karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa.
26Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu.
27Hos 14:6; Wim 2:13; Ebr 6:7Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema,
Tazama, harufu ya mwanangu
Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.
28 Ebr 11:20; Kum 33:13,28; 2 Sam 1:21; Hes 18:12; Zab 65:9; Zek 9:17 Mungu na akupe ya umande wa mbingu,
Na ya manono ya nchi,
Na wingi wa nafaka na mvinyo.
29 Mwa 9:25; 12:3; 49:8; Hes 24:9 Mataifa na wakutumikie
Na makabila wakusujudie,
Uwe bwana wa ndugu zako,
Na wana wa mama yako na wakusujudie.
Atakayekulaani alaaniwe,
Na atakayekubariki abarikiwe.
Esau Aomba Baraka30Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
31Mwa 27:4Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.
32Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.
33Mwa 28:3,4; Hes 23:20; Efe 1:3; Rum 11:29Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa.
34 Ebr 12:17 Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu.
351 The 4:6Akasema, Nduguyo amekuja kwa hila, akauchukua mbaraka wako.
36Mwa 25:29-34Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa amechukua mbaraka wangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?
37 2 Sam 8:14 Isaka akajibu, akamwambia Esau, Tazama, nimemfanya awe bwana wako, na ndugu zake wote nimempa kuwa watumishi wake; kwa nafaka na mvinyo nimemtegemeza, nami nikufanyie nini sasa, mwanangu?
38Ebr 12:17Esau akamwambia babaye, Una mbaraka mmoja tu, babangu? Unibariki mimi, mimi nami, Ee babangu. Esau akapaza sauti yake, akalia.
39 Ebr 11:20 Ebr 11:20 Isaka, baba yake, akajibu, akamwambia,
Angalia, penye manono ya nchi patakuwa makao yako,
Na penye umande wa mbingu unaotoka juu.
40 Mwa 25:23; 36:8; 2 Fal 8:20; 2 Sam 8:14; Oba 1:18-20 Kwa upanga wako wewe utaishi, nawe utamtumikia nduguyo;
Na itakuwa utakapoponyoka,
Utalivunja kongwa lake katika shingo yako.
Yakobo Akwepa Ghadhabu ya Esau41 Mwa 37:4; 50:3; Oba 1:10; 1 Yoh 3:12 Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.
42Zab 64:5Rebeka akaarifiwa maneno ya Esau, mwanawe mkubwa. Akapeleka mtu kumwita Yakobo, mwanawe mdogo, akamwambia, Tazama, katika habari zako Esau, ndugu yako, anajifariji moyo wake, maana anakusudia kukuua.
43Mwa 11:31Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani;
44ukae kwake siku chache, hata ghadhabu ya ndugu yako igeuke;
45hata ikuondokee ghadhabu ya ndugu yako, akasahau uliyomtenda. Ndipo nitakapopeleka watu kukuchukua kutoka huko. Kwa nini nifiwe nanyi nyote wawili siku moja?
46 Mwa 24:3; 26:35; 28:8 Rebeka akamwambia Isaka, Rohoni mwangu sina raha kwa sababu ya hao binti za Hethi. Kama Yakobo akitwaa mke katika binti za Hethi, kama hawa binti za nchi, maisha yangu yatanifaidia nini?
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.