Zab 45 - Swahili Union Version Bible

Wimbo wa Arusi ya KifalmeKwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Yungiyungi. Wimbo wa Wakorahi; Wimbo wa Mapenzi.

1Moyo wangu umefurika kwa neno jema,

Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme;

Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi.

2Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;

Neema imemiminiwa midomoni mwako,

Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.

3Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,

Utukufu ni wako na fahari ni yako.

4Katika fahari yako usitawi uendelee

Kwa ajili ya kweli na upole na haki

Na mkono wako wa kuume

Utakufundisha mambo ya kutisha.

5Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;

Imo mioyoni mwa adui za mfalme.

6 Ebr 1:8-9; Zab 93:2; Isa 9:6,7 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,

Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

7 Zab 33:5; Mt 3:15; Ebr 1:9; Isa 61:1; Yn 20:17 Umeipenda haki;

Umeichukia dhuluma.

Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,

Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

8Mavazi yako yote hunukia manemane

Na udi na mdalasini.

Katika majumba ya pembe

Vinubi vimekufurahisha.

9Binti za wafalme wamo

Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki.

Mkono wako wa kuume amesimama malkia

Amevaa dhahabu ya Ofiri.

10 Kum 21:13 Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,

Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.

11 Zab 95:6; Isa 54:5 Naye mfalme atautamani uzuri wako,

Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.

12Na binti Tiro analeta kipawa chake,

Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.

13 Ufu 19:7,8 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,

Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.

14Atapelekwa kwa mfalme

Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.

Wanawali wenzake wanaomfuata,

Watapelekwa kwako.

15Watapelekwa kwa furaha na shangwe,

Na kuingia katika nyumba ya mfalme.

16 1 Pet 2:9; Ufu 1:6 Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,

Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.

17 Isa 11:10; Mal 1:11 Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu

Katika vizazi vyote.

Kwa hiyo mataifa watakushukuru

Milele na milele.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help