Zab 26 - Swahili Union Version Bible

Ombi la Haki na Ungamo la WemaYa Daudi.

1 Zab 7:8; 28:7; Mit 29:25 Ee BWANA, unihukumu mimi,

Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu,

Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.

2Ee BWANA, unijaribu na kunipima;

Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.

3Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu,

Nami nimekwenda katika kweli yako.

4 Zab 1:1; Yer 15:17 Sikuketi pamoja na watu wa ubatili,

Wala sitaingia mnamo wanafiki.

5 Zab 5:5; 15:4; 31:6 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya,

Wala sitaketi pamoja na watu waovu.

6 Kut 30:19; Zab 73:13; 1 Tim 2:8 Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia,

Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA

7Ili niitangaze sauti ya kushukuru,

Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.

8BWANA, nimependa makao ya nyumba yako,

Na mahali pa maskani ya utukufu wako.

9Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,

Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.

10Mikononi mwao mna madhara,

Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.

11Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu;

Unikomboe, unifanyie fadhili.

12Mguu wangu umesimama palipo sawa;

Katika makusanyiko nitamhimidi BWANA.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help