Mt 26 - Swahili Union Version Bible

Mpango wa Kumwua Yesu

1

161 Tim 6:9,10Tokea wakati huo akawa akitafuta nafasi apate kumsaliti.

Yesu katika Pasaka pamoja na Wanafunzi

17 Mk 14:12-16; Lk 22:7-13 Kut 12:18-20 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi wake wakamwendea Yesu, wakamwambia, Ni wapi utakapo tukuandalie uile Pasaka?

18Mt 21:3Akasema, Enendeni mjini kwa mtu fulani, mkamwambie, Mwalimu asema, Majira yangu ni karibu; kwako nitafanya Pasaka pamoja na wanafunzi wangu.

19Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaagiza, wakaiandaa Pasaka.

20Mk 14:17-26; Lk 22:14-23; Yn 13:21-26Basi kulipokuwa jioni aliketi chakulani pamoja na wale Thenashara.

21Nao walipokuwa wakila, alisema, Amin, nawaambia, Mmoja wenu atanisaliti.

22Wakahuzunika sana, wakaanza kumwuliza mmoja mmoja, Ni mimi, Bwana?

23Zab 41:10Akajibu akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika kombe, ndiye atakayenisaliti.

24Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.

25Yuda, yule mwenye kumsaliti, akajibu, akasema, Ni mimi, Rabi? Akamwambia, Wewe umesema.

Kuasisiwa kwa Chakula cha Bwana

26 Mt 14:19; 1 Kor 11:23-25 Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu

27Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki;

28Kut 24:8; Yer 31:31-34; Zek 9:11kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.

29Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.

30Zab 113—118; Lk 22:39; Yn 18:1Nao walipokwisha kuimba, wakatoka nje kwenda mlima wa Mizeituni.

Yesu asema kuwa Petro Atamkana

31 Mk 14:27-31; Lk 22:31-34 Zek 13:7; Yn 16:32 Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.

32Mt 28:7,16Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.

33Petro akajibu, akamwambia, Wajapochukizwa wote kwa ajili yako, mimi sitachukizwa kamwe.

34Yn 13:38Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu.

35Mt 26:56Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana kamwe. Na wanafunzi wote wakasema vivyo hivyo.

Yesu Aomba katika Gethsemane

36 Mk 14:32-42; Lk 22:40-46 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe.

37Ebr 5:7Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka.

38Zab 43:5; Yn 12:27Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami.

39Yn 18:11; Ebr 5:8Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

40Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja?

41Ebr 2:14; 4:15Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.

42Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.

43Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito.

442 Kor 12:8Akawaacha tena, akaenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yale yale.

45Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi.

46Yn 14:31Ondokeni, twende zetuni! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia.

Kusalitiwa na Kukamatwa kwa Yesu

47 Mk 14:43-50; Lk 22:47-53; Yn 18:3-12 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Thenashara akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu.

48Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni.

49Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu.

50Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu.

51Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio.

52Mwa 9:6; Ufu 13:10Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.

53Yoe 3:11Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

54Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?

55Lk 19:47; 21:37Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka kama kumkamata mnyang’anyi, wenye panga na marungu, ili kunishika? Kila siku naliketi hekaluni nikifundisha, msinikamate.

56Mt 26:31Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.

Yesu mbele ya Kuhani Mkuu

57 Mk 14:53-72; Lk 22:54-71; Yn 18:12-27 Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.

58Na Petro akamfuata kwa mbali mpaka behewa ya Kuhani Mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.

59Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;

60wasiuone wangawa walitokea mashahidi wa uongo wengi.

61Yn 2:19-21Hata baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.

62Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini?

63Mt 27:12Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

64Dan 7:13; Zab 110:1; Mt 16:27; 24:30Yesu akamwambia, Wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.

65Law 24:16; Mt 9:3; Yn 10:33Ndipo Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; mna haja gani tena ya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake;

66Yn 19:7mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kuuawa.

67Isa 50:6Ndipo wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde; wengine wakampiga makofi,

68wakisema, Ewe Kristo, tufumbulie; ni nani aliyekupiga?

Petro Amkana Yesu

69Na Petro alikuwa ameketi nje behewani; kijakazi mmoja akamwendea, akasema, Wewe nawe ulikuwapo pamoja na Yesu wa Galilaya.

70Akakana mbele ya wote, akisema, Sijui usemalo.

71Naye alipotoka nje hata ukumbini, mwanamke mwingine alimwona, akawaambia watu waliokuwako huko, Huyu alikuwapo pamoja na Yesu Mnazareti.

72Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.

73Punde kidogo, wale waliohudhuria wakamwendea, wakamwambia Petro, Hakika wewe nawe u mmoja wao; kwa sababu hata usemi wako wakutambulisha.

74Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara akawika jogoo.

75Mt 26:34Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help