Yn 2 - Swahili Union Version Bible

Harusi ya Kana

1 Yn 1:43 Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo.

2Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake.

3Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, Hawana divai.

4Yn 19:26; Mt 12:48; Mk 1:24Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.

5Mamaye akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambia, fanyeni.

6Mk 7:3,4Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu.

7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu.

8Akawaambia, Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza. Wakapeleka.

9Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi,

10akamwambia, Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa.

11Yn 1:14; 11:40Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.

12 Mt 4:13; Yn 7:3 Baada ya hayo akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake; wakakaa huko siku si nyingi.

Yesu Atakasa Hekalu

13 Kut 12:1-27 Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu; naye Yesu akakwea mpaka Yerusalemu.

14Mt 21:12,13; Mk 11:15-17; Lk 19:45,46Akaona pale hekaluni watu waliokuwa wakiuza ng’ombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi.

15Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao;

16Lk 2:49akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.

17Zab 69:9Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako utanila.

18Mt 21:23; Yn 3:2Basi Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara gani utuonyeshayo, kwamba unafanya haya?

19Mt 26:61; 27:40; Mk 14:58; 15:29Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hili, nami katika siku tatu nitalisimamisha.

20Basi Wayahudi wakasema, Hekalu hili lilijengwa katika muda wa miaka arobaini na sita, nawe utalisimamisha katika siku tatu?

211 Kor 6:19Lakini yeye alinena habari za hekalu la mwili wake.

22Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.

23Hata alipokuwapo Yerusalemu kwenye sikukuu wakati wa Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoziona ishara zake alizozifanya.

24Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;

25Mk 2:8na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help