Zab 116 - Swahili Union Version Bible

Shukrani kwa Kuponywa Maradhi

1Haleluya.

Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza

Sauti yangu na dua zangu.

2Kwa maana amenitegea sikio lake,

Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.

3Kamba za mauti zilinizunguka,

Shida za kuzimu zilinipata.

Naliona taabu na huzuni;

4Nikaliitia jina la BWANA.

Ee BWANA, nakuomba sana,

Uniokoe nafsi yangu.

5 Ezr 9:15; Neh 9:8; Zab 11:7; Yer 12:1; Omb 1:18; Ufu 16:5 BWANA ni mwenye neema na haki,

Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.

6BWANA huwalinda wasio na hila;

Nalidhilika, akaniokoa.

7 Yer 6:16; Mt 11:29 Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako,

Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

8Maana umeniponya nafsi yangu na mauti,

Macho yangu na machozi,

Na miguu yangu na kuanguka.

9Nitaenenda mbele za BWANA

Katika nchi za walio hai.

10 2 Kor 4:13 Naliamini, kwa maana nitasema,

Mimi naliteswa sana.

11 2 Fal 4:16; Yer 9:5; Rum 3:4 Mimi nalisema kwa haraka yangu,

Wanadamu wote ni waongo.

12Nimrudishie BWANA nini

Kwa ukarimu wake wote alionitendea?

13Nitakipokea kikombe cha wokovu;

Na kulitangaza jina la BWANA;

14 Zab 22:25; Yon 2:6 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,

Naam, mbele ya watu wake wote.

15 Ayu 5:26; Zab 72:14; Lk 16:22; Ufu 14:13 Ina thamani machoni pa BWANA

Mauti ya wacha Mungu wake.

16Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako,

Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako,

Umevifungua vifungo vyangu.

17Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;

Na kulitangaza jina la BWANA;

18Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA,

Naam, mbele ya watu wake wote.

19Katika nyua za nyumba ya BWANA,

Ndani yako, Ee Yerusalemu.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help