Ebr UTANGULIZI - Swahili Union Version Bible

UTANGULIZIWaraka huu hautaji jina la mwandishi, walengwa wake wala mahali ulikotumwa. Hata hivyo, kutokana uandishi wake, inaonekena kwamba mwandishi huyo aliwaandikia Wakristo walioongoka kutoka dini ya Kiyahudi na ambao imani yao ilikuwa inafifia. Anawatia moyo wasikate tamaa kwa kuwa Kristo ametimiza yote yaliyotakiwa katika Agano la Mungu.Kwa namna ya pekee kabisa mwandishi anazingatia kuonyesha hali ya pekee ya Yesu, Mwana wa Mungu: yeye ni mkuu kuliko vitu vyote (1:2-4), mkuu juu ya malaika (1:4–2:18), mkuu kuliko Musa (3:1–4:13) au ukuhani wa Walawi (4:14–7:28). Yesu ni Kuhani Mkuu ambaye alipenyeza mpaka mbinguni (4:14) na ambaye kwa damu yake alitufungulia njia mpya na hai “tupate kuingia katika mahali patakatifu mno” (10:19-20). Wakati Torati ya Musa na ibada za Agano la Kale zilipofanyika mara nyingi pamoja na taratibu zake za sadaka nyingi na ibada zilizokuwa ngumu sana kuelewa, Kristo alichukua mwili wake mwenyewe kama sadaka iliyofanyika “mara moja tu milele” (9:26-28; 10:10,14), akawa mdhamini (7:22) wa Agano Jipya la daima.Baada ya kueleza ukuu wake Yesu Kristo, katika sura 10:19–13:17 mwandishi anawahimiza walengwa wake wadumu imara kwa kuwapa, baadhi ya mengineyo, mifano kutoka Agano la Kale ya watu waliodumu katika imani.
Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help