1Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,
Umekuwa na hasira, uturudishe tena.
2Umeitetemesha nchi na kuipasua,
Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.
3Umewaonyesha watu wako mazito,
Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.
4 Isa 11:10 Umewapa wakuogopao bendera,
Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.
5 Zab 108:6 Ili wapenzi wako waopolewe,
Uokoe kwa mkono wako wa kuume, utuitikie.
6 Zab 89:35; Mwa 12:6; Yos 13:27 Mungu amenena kwa utakatifu wake,
Nami nitashangilia.
Nitaigawanya Shekemu,
Nitalipima bonde la Sukothi.
7 Kum 33:17; Mwa 49:10 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,
Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.
Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
8Moabu ni bakuli langu la kunawia.
Nitamtupia Edomu kiatu changu,
Na kumpigia Filisti kelele za vita.
9Ni nani atakayenipeleka hata mji wenye boma?
Ni nani atakayeniongoza hata Edomu?
10 Zab 44:9 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?
Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?
11Utuletee msaada juu ya mtesi,
Maana wokovu wa binadamu haufai.
12 1 Nya 19:13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,
Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.