1 Mhu 5:8; Kut 21:6 Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu;
Katikati ya miungu anahukumu.
2 Kum 1:17; Zab 58:1,2 Hata lini mtahukumu kwa dhuluma,
Na kuzikubali nyuso za wabaya?
3Mfanyieni hukumu maskini na yatima;
Mtendeeni haki aliyeonewa na fukara;
4Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
5 Zab 11:3 Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani;
Misingi yote ya nchi imetikisika.
6 Ayu 21:32; Eze 31:14; Yn 10:34 Mimi nimesema, Ndinyi miungu,
Na wana wa Aliye juu, nyote pia.
7Lakini mtakufa kama wanadamu,
Mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
8 Zab 2:8; Ufu 11:15 Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi,
Maana Wewe utawarithi mataifa yote.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.