1 Kol 3:20 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2Kut 20:12; Kum 5:16Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
4Kol 3:21; Isa 50:5; Mit 2:2; 3:11; 19:18; Kum 6:7,20-25; Zab 78:4Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
Watumwa na Mabwana5 Kol 3:22-25; Tit 2:9,10; 1 Pet 2:18 Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;
6wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;
7kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;
82 Kor 5:10mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.
9Kum 10:17; Kol 3:25; 4:1; 2 Nya 19:7; Mdo 10:34Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo.
Silaha zote za Mungu10 1 Kor 16:13; 1 Yoh 2:14 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11Efe 4:14; 2 Kor 10:4Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12Efe 2:2; Yn 14:30; Kol 1:13; 1 Pet 5:8,9Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
131 Fal 20:11Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14Isa 11:5; 59:17; Lk 12:35; 1 Pet 1:13; 1 The 5:8Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15Isa 52:7; 40:3,9na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
161 Pet 5:9; 1 Yoh 5:4zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17Isa 59:17; 11:4; 49:2; 51:16; 1 The 5:8; Hos 6:5Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18Mt 26:41; Kol 4:2,3kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
19Kol 4:3; 2 The 3:1; Mdo 4:29pia na kwa ajili yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri ile siri ya Injili;
202 Kor 5:20; Kol 4:4ambayo kwa ajili yake mimi ni mjumbe katika minyororo; hata nipate ujasiri katika huyo kunena jinsi inipasavyo kunena.
Mambo ya Kibinafsi na Baraka21 Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Kol 4:7 Kol 4:7-8 Basi ninyi nanyi mpate kuzijua habari zangu, ni hali gani, Tikiko, ndugu mpendwa, mhudumu mwaminifu katika Bwana, atawajulisheni mambo yote;
22Kol 4:7,8ambaye nampeleka kwenu kwa kusudi lilo hilo mpate kuzijua habari zetu, naye awafariji mioyo yenu.
23Amani na iwe kwa ndugu, na pendo, pamoja na imani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo.
241 Pet 1:8Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana wetu Yesu Kristo katika hali ya kutokuharibika.
Who We AreWhat We EelieveWhat We Do
2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.