Hes 2 - Swahili Union Version Bible

Amri ya Kupiga Kambi na Kuingia

1BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

2Hes 1:52; 24:2-9Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye beramu yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote.

3Hes 10:14; Rut 4:20; 1 Nya 2:10; Mt 1:4; Lk 3:32,33Na hao watakaopanga upande wa mashariki, kwa kuelekea maawio ya jua, ndio wale wa beramu ya marago ya Yuda, kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Yuda atakuwa Nashoni mwana wa Aminadabu.

4Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sabini na nne elfu na mia sita.

5Hes 7:18,23Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Isakari; na mkuu wa wana wa Isakari atakuwa Nethaneli mwana wa Suari;

6Hes 26:25na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na nne elfu na mia nne;

7Mwa 49:13; Kum 33:18na kabila ya Zabuloni; na mkuu wa wana wa Zabuloni atakuwa Eliabu mwana wa Heloni;

8na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na saba elfu na mia nne.

9Hes 10:14; 1 Nya 5:2; Zab 78:52Hao wote waliohesabiwa katika marago ya Yuda walikuwa mia na themanini na sita elfu na mia nne, kwa majeshi yao. Hao ndio watakaosafiri mbele.

10 Kum 33:6; 1 Nya 5:1 Upande wa kusini kutakuwa na beramu ya marago ya Reubeni kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Reubeni atakuwa Elisuri mwana wa Shedeuri.

11Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na sita elfu na mia tano.

12Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Simeoni; na mkuu wa wana wa Simeoni atakuwa Shelumieli mwana wa Suri-shadai;

13na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na kenda elfu na mia tatu;

14na kabila ya Gadi; na mkuu wa wana wa Gadi atakuwa Eliasafu mwana wa Deueli;

15na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na tano elfu na mia sita na hamsini.

16Hes 10:18; Mwa 49:3; 1 Nya 5:1Wote waliohesabiwa katika marago ya Reubeni walikuwa mia na hamsini na moja elfu na mia nne na hamsini, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri mahali pa pili.

17 Mdo 7:44; Ebr 8:2; 1 Kor 14:40 Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na marago ya Walawi katikati ya marago yote; kama wapangavyo marago, watasafiri vivyo, kila mtu mahali pake, penye beramu zao.

18 Mwa 48:14-20; Zab 80:1; Hos 11:3 Upande wa magharibi kutakuwa na beramu ya marago ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.

19Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa arobaini elfu na mia tano.

20Na karibu naye itakuwa kabila ya Manase; na mkuu wa wana wa Manase atakuwa Gamalieli mwana wa Pedasuri;

21na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na mbili elfu na mia mbili;

22Zab 68:27; Ufu 7:8tena kabila ya Benyamini; na mkuu wa wana wa Benyamini atakuwa Abidani mwana wa Gideoni;

23na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa thelathini na tano elfu na mia nne.

24Hes 10:22Wote waliohesabiwa katika marago ya Efraimu walikuwa mia na nane elfu na mia moja, kwa majeshi yao. Nao ndio watakaosafiri katika mahali pa tatu.

25 Kum 32:22 Upande wa kaskazini kutakuwa na beramu ya marago ya Dani kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Dani atakuwa Ahiezeri mwana wa Amishadai.

26Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa sitini na mbili elfu na mia saba.

27Na hao watakaopanga karibu naye ni kabila ya Asheri; na mkuu wa wana wa Asheri atakuwa Pagieli mwana wa Okrani;

28na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa arobaini na moja elfu na mia tano;

29Mwa 30:8; 49:21; 2 Fal 15:29; Ufu 7:6kisha kabila ya Naftali; na mkuu wa wana wa Naftali atakuwa Ahira mwana wa Enani;

30na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa hamsini na tatu elfu na mia nne.

31Hes 10:25Wote waliohesabiwa katika marago ya Dani walikuwa mia na hamsini na saba elfu na mia sita. Hao ndio watakaosafiri mwisho kwa kuandama beramu zao.

32 Kut 12:37; 38:26; Hes 1:46; 11:21 Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli kwa nyumba za baba zao; wote waliohesabiwa katika marago kwa majeshi yao, walikuwa mia sita na tatu elfu na mia tano na hamsini.

33Hes 1:47; 26:57-62Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwagiza Musa.

34Kut 39:42; Hes 24:2,9; Zab 119:6; Isa 45:12; Lk 1:6; 1 Kor 14:40Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyopanga penye beramu zao, na ndivyo walivyosafiri, kila mtu kwa jamaa zao, kwa nyumba za baba zao.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help