Zab 17 - Swahili Union Version Bible

Sala ya Ukombozi kutoka kwa WatesajiOmbi la Daudi.

1Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu,

Utege sikio lako kwa maombi yangu,

Yasiyotoka katika midomo ya hila.

2Hukumu yangu na itoke kwako,

Macho yako na yatazame mambo ya adili.

3 Ayu 23:10; Yak 3:2 Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku,

Umenihakikisha usione neno;

Nimenuia kinywa changu kisikose,

4 Rum 12:2 Mintarafu matendo ya wanadamu;

Kwa neno la midomo yako

Nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

5Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,

Hatua zangu hazikuondoshwa.

6Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,

Utege sikio lako ulisikie neno langu.

7Dhihirisha fadhili zako za ajabu

Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;

Kwa mkono wako wa kuume

Uwaokoe nao wanaowaondokea.

8 Kum 32:10 Unilinde kama mboni ya jicho,

Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;

9Wasinione wasio haki wanaonionea,

Adui za roho yangu wanaonizunguka.

10Wameukaza moyo wako,

Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.

11 1 Sam 23:26 Sasa wametuzunguka hatua zetu,

Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.

12Kama mfano wa simba atakaye kurarua,

Kama mwana-simba aoteaye katika maoteo yake.

13Ee BWANA, usimame, umkabili, umwinamishe,

Kwa upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.

14Ee BWANA, kwa mkono wako uniokoe na watu,

Watu wa dunia hii ambao fungu lao li katika maisha haya.

Matumbo yao wayajaza kwa hazina yako,

Hushiba wana, huwaachia watoto wao akiba zao,

15 Ayu 19:26,27; Kol 1:15 Bali mimi nikutazame uso wako katika haki,

Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.

Blog
About Us
Message
Site Map

Who We AreWhat We EelieveWhat We Do

Terms of UsePrivacy Notice

2025 by iamachristian.org,Inc All rights reserved.

Home
Gospel
Question
Blog
Help